We have 132 guests and no members online

Majeshi ya Syria yadhibiti mji wa Al-Bukamal kutoka mikononi mwa IS

Posted On Thursday, 09 November 2017 05:52 Written by
Rate this item
(0 votes)

media

Askari wa jeshi la Syria (Hapa ilikua Deir Ezzor Oktoba 31, 2017).

Majeshi ya Syria yakisaidiwa na kundi la Hezbollah kutoka Lebanon na wanamgambo wa Iraq wameurejesha tangu siku ya Jumatano jioni mji wa Al-Bukamal kwenye himaya ya serikali kutoka mikononi mwa kundi la Islamic State.

Al-Bukamal ni mji wa mwisho ambao ulikua ukishikiliwa na kundi la Islamic State mashariki mwa Syria. Taarifa ya kuurejesha mji huu kwenye himaya ya serikali imethibitishwa na vyanzo vya serikali vya Syria na shirika la la habari la Urusi la Sputnik.

Jeshi la Syria lilitarajia vita vikali na vya muda mrefu kwa minajili ya kuurejesha kwenye himaya yake mji wa Al-Bukamal, ambapo walikua walijificha wapiganaji wa mwisho wa kundi la Islamic State, ambao walikimbia mkoa wa Syria wa Deir Ezzor na mji wa Iraq wa Al-Qaim. Lakini wapiganaji hao wamepoteza mji huo kwa haraka kuliko ilivyotarajiwa.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kijeshi kutoka Syria, Urusi na Syria walitumia uwezo mkubwa katika vita vya kuurejesha mji huo kwenye himaya ya serikali. Kikosi cha wanamaji na kile cha wanaanga walirusha makombora mengi na mabomu wiki mbili zilizopita dhidi ya ngome za kundi la Islamic Islamic.

Pamoja na kupoteza mji wa Al-Bukamal, kundi la Islamic State halina tena mji wowote linaloshikilia nchini Iraq na Syria. Lakini wapiganaji wa kundi hilo wapo katika maeneo makubwa ya jangwani kati ya nchi hizo mbili, ambako wamehifadhi chakula, silaha, na risasi, kwa kutarajia vita ya vya kuvizia katika nchi hizo.

Chanzo:RFI

Read 67 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli