We have 125 guests and no members online

SERIKALI KUPIMA UTENDAJI KAZI WA MAAFISA UGANI NCHINI

Posted On Sunday, 19 November 2017 02:53 Written by
Rate this item
(0 votes)

Serikali imewataka Watendaji na Maafisa Ugani mkoani hapa kutoka Maofisini na kwenda kwa wakulima kwa ajili ya kuwaelekeza na kuwaelimisha juu ya kilimo bora kitakachowawezesha kupata mazao bora yatakayowapa faida kubwa.

Kauli hiyo imetolewa mjini Tabora na Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais , Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa( TAMISEMI ) Tixon Nzunda wakati akizungumza na Watendaji  na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Manispaa ya Tabora , Halmashauri za Wilaya ya Sikonge, Uyui , Kaliua na Urambo.

Alisema kuwa ili kufikia lengo hilo inatakiwa kuanzia hivi sasa Wakurugenzi wote waandae rejista(Daftari maalumu) litakalomwonyesha aina ya huduma ambayo Afisa Ugani aliyotoa kwa Mkulima, siku ya utoaji wa huduma hiyo, Jina la kijiji na la Mkulima aliyepatiwa huduma , idadi ya wakulima aliwahudumia katika msimu mzima wa kilimo na  Afisa Mtendaji au Mwenyekiti wa Kijiji husika.

Nzunda alisema kuwa msimu wa kilimo umeanza katika maeneo mbalimbali ni vema utaratibu huo ukaanza kutumia ili kuondoa tabia ya Maofisa Ugani kushinda Maofisini bali waende vijijini kutekeleza majukumu ya kuwasaidia wakulima ili waweze kuzalisha kwa tija kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa baada ya kisicho kirefu atafuatilia kama kweli utaratibu huo umeanza kutekelezwa na endapo itabainika Mtendaji yoyote kukaidia atalazimika kumcukulia hatua kwa sababu atakuwa hana nia njema na wakulima wa nchi hii kwa sababu anataka waendelee kulima kilimo duni.

Nzunda alisisitiza kuwa Afisa Ugani anapaswa kuwa mfano kwa kwenda kwa wakulima na kuwa na shamba darasa ambalo wakulima watakwenda kwake kuchota ujuzi na sio kutoa maelekezo akiwa ofisini.

Alisema kuwa Mkoa wa Rukwa uliweza kufanikiwa kuzalisha mazao mengi na kupata ziada ya kutosha kupitia utaratibu huu wa kubanana na Maafisa Ugani ni vema maeneo mengine nchini nayo yakaiga utaratibu huu kwani uwasaidia wakulima na Mamlaka ya Serikali za Mitaa katika kuongeza mapato yake.

Katika hatua nyingine Naibu Katibu Mkuu huyo ameagiza viongozi na watendaji mbalimbali kuhakikisha pembejeo zote zinauzwa katika bei elekezi ya Serikali ili kuepusha wakulima kutapeliwa.

Alisema ikibainika mtu kuuza nje ya utaratibu wa bei elekezi ya Serikali ni vema akachukuliwa hatua ili asiendelee kuwaumiza wakulima na kuwasababisha kubeba mzigo mkubwa ambao hawezi kumpa tija wakati wa uzalishaji kwa kuwa atakuwa ametumia pesa nyingi faida kidogo.

Naibu Katibu Mkuu yupo katika ziara ya kikazi katika Mikoa ya Kigoma, Tabora na Singida kwa lengo ya kuhimiza usimamizi bora wa sekta ya elimu , kilimo, mifugo , utawala bora na mengine mengi.

Na Tiganya Vincent, Tabora

Read 42 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli