We have 125 guests and no members online

Zanu-PF kuanzisha mchakato wa kumng'oa Mugabe mamlakani

Posted On Tuesday, 21 November 2017 11:45 Written by
Rate this item
(0 votes)

media

Mmoja wa waandamanaji katika mitaa ya Harare, Jumamosi, Novemba 18, 2017.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameendelea kushikilia msimamo wake wa kusalia madarakani, licha ya shinikizo kutoka pande zote nchini humo kumtaka ajiuzulu mara moja. Kwa mujibu wa jeshi, Mugabe amekua akiwasiliana na aliyekua makamu wake Emmerson Mnangagwa.

Hata hivyo Chama cha Zanu-PF kinatarajia hii leo kuanzisha mchakato wa kumtimua madarakani. Lakini Mkuu wa majeshi, Jenerali Constantino Chiwenga amezitaka pande husika katika mchakato wa kumuondoa madarakani rais Mugabe kusalia watilivu.

Katika hotuba yake kwenye televisheni, Jenerali Chiwenga alisema ameridhishwa na "maendeleo mapya" tangu mapinduzi ya kijeshi wiki iliyopita, hususan "mawasiliano kati ya rais Mugabe na aliyekua makamu wake Emmerson Mnangagwa, ambaye anatarajiwa hivi karibuni nchini Zimbabwe".

Mkuu wa majeshi ya Zimbabwe, Jenerali Constantino Chiwenga (katikati), Harare, Novemba, 20, 2017.

"Sisi, vikosi vya usalama na ulinzi vya Zimbabwe tunawahimiza wananchi wa Zimbabwe kusalia watulivu, na kuheshimu sheria za nchi", pia alisema Jenerali Constantino Chiwenga katika hotuba yake, siku moja kabla ya maandamano mapya dhidi ya Robert Mugabe, madarakani kwa miaka 37.

Afisa wa Zanu-PF amesema kuwa hoja ya kumnyang'anya urais itawasilishwa bungeni leo Jumanne na mchakato wa kumng'oa madarakani unaweza kuchukua siku mbili tu.

Mashtaka yaliyomo kwenye hoja hiyo ni pamoja na kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 "kumpa madaraka makubwa ya kikatiba mkewe Grace, na kushindwa kuheshimu katiba''.

Emmerson Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 75, aliachishwa kazi tarehe 6 Novemba na kulazimika kukimbilia uhamishoni baada mvutano na mkewe rais Mugabe, Grace Mugabe, mwenye umri wa miaka 52, ambaye alifanikiwa kumuondoa hasimu wake katika kinyang'anyiro cha kumrithi mumewe.

Tangu wakati huo, jeshi limekua na mazungumzo na rais Mugabe anaekataa kujiuzulu licha ya shinikizo kutoka pande mbalimbali nchini Zimbabwe.

Chanzo:RFI

Read 42 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli