We have 135 guests and no members online

JAMII YATAKIWA KUHAKIKISHA KILA MAMA ANAJIFUNGULIA KATIKA VITUO VYA AFYA

Posted On Wednesday, 22 November 2017 07:00 Written by
Rate this item
(0 votes)

Katika kuhakikisha Vifo vinavyotokana na uzazi kwa kina Mama vinapungua, Jamii imehimizwa kumpeleka mzazi kwenda kwenye vituo vya Afya ambavyo vina wataalamu, kwani hatua hiyo ndio njia ya kusaidia kuondokana vifo hivyo.

Hayo yamebainishwa na Mratibu Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe na Uzazi Salama, Rose Mlay wakati wa mkutano wa wadau wakati wa Mkutano wa Wadau wa Afya na Mama na Mtoto uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kupoteza mtoto na mama ni ajali ambayo inatokana na kukosekana kwa huduma sahihi wakati wa kujifungua.

Amesema kuwa mkutano wadau ni pamoja na kujadili takwimu za Afya ya Mama na Mtoto pamoja na kuweka mikakati ya kupunguza vifo vya uzazi.

Mlay amesema kwa sasa vifo vya wakina Mama vimeongezeka kutoka kwa vifo 24 vya wakinamama kwa siku hadi kufikia vifo 30 kwa siku huku akisema ongezeko hilo limechangiwa na wakina Mama kujifungulia sehemu zisizo salama,

“Ripoti inaonyesha vifo vinaongezeka kutokana na kukosekana kwa vituo vya afya vyenye pamoja na wataamu kama nyumbani na kwenye vituo visivyo na watalaamu,unakuta sehemu hakuna vifaa vya kumsaidia Mama ili aweze kujifungua salama,na hii inasababisha vifo hivi kuongekezeka”

“.Amesema jamii kama ingekuwa inampeleka Mzazi kwenye vituo vya afya vyenye ubora basi vifo hivi vingepungua ikiwezekana kumalizika kabisa”Amesema Mlay.

Mlay amesema Takwimu za hapo awali zilionyesha kuwa takribaniwanawake 8000 hufaliki kila mwaka kwa sababu ya Matatizo yanayotokana na Mimba na Uzazi lakini Takwimu hizo zimeongekeza hadi kufikia zaidia ya elfu 10 kwa mwaka .

Kwa upande wao Wadau mbalimbali waliokuwepo kwenye Mkutano huo ,wameitaka serikali kuhakikisha inaongeza bajeti kwenye sekta ya Afya ambayo itavisaidia kwenye vituo vya Afya kuwepo kwa wakunga wenye welevu na ujuzi ambao watasaidia kupunguza vifo hivo.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Read 52 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli