We have 145 guests and no members online

Aliekuwa makamu wa rais kumrithi Mugabe

Posted On Wednesday, 22 November 2017 07:01 Written by
Rate this item
(0 votes)

media

Emmerson Mnangagwa wakati wa hotuba ya Robert Mugabe kwa taifa mbele ya Bunge, Agosti 25, 2015.

Aliyekuwa makamu wa rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ambaye alifutwa kazi wiki tatu zilizopita na kutoroka nchi hiyo kufuatia vitisho vya kifo , anatazamia kurejea nchini leo Jumatano mchana, siku moja baada ya rais Robert Mugabe kujiuzulu, na kuongoza Zimbabwe kwa muda kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Emmerson Mnangagwa anatazamia kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi baada ya kuteuliwa katika mkutano wa hadhara wa chama cha Zanu-PF siku ya Jumapili kuongoza chama hicho tawala.

Zanu-PF, chama cha Robert Mugabe kilimtaka aachie ngazi vinginevyo Spika wa Bunge ataanzisha utaratibu wa kumng'atua mamlakani.

Kulingana na katiba ya nchi ya Zimbabwe rais anapojiuzulu makamu wake ndio anachukua nafasi yake hadi uchaguzi mpya.

Bw. Mnangagwa atatawazwa kesho Alhamisi na hivyo kuanza rasmi majukumu ya uongozi wa taifa la Zimbabwe, baada ya miaka 37 ya uongozi wa Robert Mugabe.

Maelfu ya raia wa Zimbabwe walimiminika katika mitaa ya miji mbalimbali baada ya tangazo la kujiuzulu kwa rais Robert Mugabe.

Waandamanaji katika mitaa ya Johannesburg, Afrika Kusini, wakifurahia kujiuzulu kwa Robert Mugabe Novemba 21, 2017.

Mchakato wa kumtimua Rais Robert Mugabe ulikua ulianza bungeni saa chache kabla ya hatua yake ya kujuzulu.

Raia wa Zimbabwe wanaamini kuwa, kujiuzulu kwa Mugabe ni mwamko mpya kwa nchi yao kiuchumi na kisiasa.

Emmerson Mnagangwa, anatarajiwa kuongoza kwa muda kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Jeshi nchini humo lilianzisha mchakato wa kukosa imani na uongozi wa Mugabe baada ya mkewe Grace, kuonekana kuingilia uongozi wake.

Chanzo:RFI

Read 93 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli