We have 126 guests and no members online

MATAWI YA BENKI YA EXIM YAPATA UTHIBITISHO WA KIMATAIFA

Posted On Friday, 24 November 2017 05:58 Written by
Rate this item
(0 votes)

Katika jitihada zake za kuwa benki yenye uvumbuzi na ufanisi, benki ya Exim Tanzania imekuwa benki ya kwanza nchini kwa matawi yake kupata cheti cha ISO 9001:2015 ikiwa kama uthibitisho wa ubora wa kimataifa kutoka shirika la viwango la kimataifa (International Standard Organization)

Shirika la ISO limejikita katika kuweka viwango vya ubora wa kimataifa ambavyo vinatokana na kanuni za usimamizi za ubora ikiwemo kujikita katika kuboresha huduma kwa wateja, kuangalia msukumo na hamasa ya viongozi wa juu wa mashirika, jinsi michakato na operesheni zinavyoendeshwa na kuboreshwa.

Akizungumza wakati wa hafla ya kupokea cheti hicho katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa rasilimali watu wa benki ya Exim, Fredreick Kanga alisema kuwa uthibitisho huo kutoka ISO ni moja ya hatua kubwa ambazo benki hiyo imepiga kimafanikio ikiwa benki iliyopata tuzo hivi karibuni kutoka Banker – Afrika Mashariki ya kuwa benki bora kwa wateja binafsi.

Mkuu wa rasilimali watu wa benki ya Exim, Fredreick Kanga akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu matawi ya benki hiyo kupata cheti cha ISO 9001:2015 ikiwa kama uthibitisho wa ubora wa kimataifa kutoka shirika la viwango la kimataifa (International Standard Organization)

“Kupata uthibitisho huu kutoka ISO ni hatua muhimu katika kuonyesha msimamo wetu wa kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wetu. Lengo letu ni kuendelea kuboresha Imani katika soko, kwa wateja wetu, kuboresha utoaji huduma, kupunguza muda wa kutoa huduma, kuwa tofauti na benki nyingine, kuongeza ufanisi na pia kupata faida na kuongeza soko letu,” aliendelea Bwana Frederick Kanga.

Mchakato wa kupata cheti hicho cha ISO ulianza mwaka huu ambapo matawi ya benki hiyo ya Exim Tower, Clock Tower na Namanga yaliteuliwa kuwa ndiyo ya kwanza kupitia mchakato huo.

Mradi huo ambao umechukua miezi takribani sita, ulianza kwa kutoa mafunzo husika kwa wafanyakazi juu ya kanuni za usimamizi ubora wa ISO 2001:2015, pia uboreshwaji wa viwango, ukaguzi wa ndani, utengenezaji wa ratiba ya matukio, kuweka mipango muhimu hadi kufikia upatikanaji wa uthibitisho huo na ilikuwa kujitoa kwao na utendaji bora ambao umesababisha tuzo hii.

Mwakilishi wa shirika la viwango la kimataifa (International Standard Organization-ISO), Nyasha Mupukuta akizungumza kuhusu cheti cha uthibitisho wa ubora wa kimataifa ambacho wamekitoa kwa matawi ya benki ya Exim.

Pia akizungumza katika hafla hiyo mwakilishi wa ISO Tanzania alisema kuwa shirika hilo lilianzishwa likiwa na dhumuni la kujibu swali la “Je ipi ni njia bora zaidi ya kufanya jambo?”

“ISO imetengeneza viwango vinavyozingatia kila sekta na hivyo basi kampuni inapopata kuthibitishwa na ISO ina maana kuwa watumiaji wanaweza kuwa na uhakika na imani kwamba bidhaa wanazonunua ni salama, za kuaminika na za ubora wa hali ya juu,” aliongeza mwakilishi huyo wa ISO.

Benki ya Exim bank imejikita katika kujenga chapa bora iliyoenea kijiografia, kuwa na bidhaa za kivumbuzi, mahusiano bora na uwezo wa kutoa huduma kwa haraka. Kwa kupata uthibitisho huu wa ubora wa viwango benki inategemea kuwa na ukaguzi wa ndani na nje unaofanyika mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa operesheni za kibenki na taratibu zilizowekwa zinafuatwa ili kuhakikisha utoaji huduma wenye ubora wa hali ya juu kwa wateja.

Mwakilishi wa shirika la viwango la kimataifa (International Standard Organization-ISO), Nyasha Mupukuta akimakbidhi cheti cha ISO 9001:2015 Mkuu wa rasilimali watu wa benki ya Exim, Fredreick Kanga.

Mkuu wa Rasilimali watu wa benki ya Exim alimalizia kwa kusema kuwa, “Tukiwa kama benki yenye uthibitisho wa ISO tutaendelea kuhakikisha utoaji wa huduma na bidhaa bora, ubora wa kuridhika kwa wateja wetu, kupunguza gharama za uendeshaji, ufanisi katika operesheni, uboreshaji wa mawasiliano, kuongezeka kwa hamasa kwa wafanyakazi na mwongezeko wa mauzo na masoko.”

Benki ya Exim pia inategemea kupata faida za ndani na nje ya nchi, kuwepo na mtazamo wa ubora wa juu, kuwepo na ufahamu mzuri kwa wafanyakazi, mapungufu ya malalamiko ya wateja, kupungua kwa hitilafu, kukubalika kwa huduma na bidhaa kimataifa na hivyo marejesho mazuri katika uwekezaji wetu.

Read 27 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli