We have 144 guests and no members online

Ibrahim Class awapa Watanzania kile walichotarajia

Posted On Sunday, 26 November 2017 08:16 Written by
Rate this item
(0 votes)

Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimpongeza Bondia Ibrahim Class baada ya kuibuka mshindi katika pambano la ngumi la kimataifa lenye mizunguko kumi na mbili dhidi ya Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yusuph Singo.

Na Shamimu Nyaki-WHUSM.

Mwanamasumbwi Ibrahim Class amewapa raha watanzania jana Jijini Dar es Salaam baada ya kumpiga Bondia Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini katika mtanange wa kimataifa baina yao uliokuwa na mizunguko kumi na mbili.

Katika pambano hilo lililohuzuriwa na Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, Ibrahim Class alishinda katika mzunguko wa kumi na mbili ambapo ameandika historia ya muda mrefu hapa nchini kwa mabondia kutofanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa.

Akizungumza baada ya mchezo huo kumalizika Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema amefurahiswa sana na ushindi aliopata Ibrahim Class na kuahidi kumpa ushirirkiano zaidi ili aendelee kufanya vizuri katika mashindano mengine

“Siri ya mafanikio katika Michezo ni kufanya mazoezi,kujiamini kusikiiza mafundisho ya mwalimu pamoja na nidhamu,Ibrahim Class ni mwanamasumbwi anaepaswa kuigwa na mabondia na wanamichezo wengine wote kutokana na uwezo wake wa kujituma hivyo wanamichezo wanapaswa kuiga kutoka kwake ili wafanikiwe na kuitangaza nchi yetu kimichezo.” Alisema Dkt. Mwakyembe.

Naye bondia Ibrahim Class ameishukuru Serikali kwa ushirikiano iliyompa wakati wa mazoezi mpaka leo amefanikiwa kupeperusha vyema Bendera ya Tanzania na ameahidi kuendelea kufanya vizuri zaidi kila atakapokuwa ulingoni na kushinda mataji na mikanda mingi zaidi.

Read 80 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji