We have 135 guests and no members online

BENKI YA EXIM YATOA MSAADA WA VITANDA NA MAGODORO KWA HOSPITALI YA RUFAA DODOMA

Posted On Wednesday, 29 November 2017 04:24 Written by
Rate this item
(0 votes)

Benki ya Exim imetoa msaada wa vitanda na magodoro 40 kwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwa ni muendelezo wa kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwake.

Hospitali hiyo ya rufaa ya Dodoma imekuwa ya nne kupokea msaada baada ya Hospitali ya Ligula, Mtwara mwezi uliopita, Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar mwezi Septemba na Hospitali ya
rufaa Temeke, Dar es Salaam mwezi wa nane mwaka huu lengo likiwa ni kutoa vitanda na magodoro 500 katika hospitali za serikali katika mikoa 13 nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa idara ya masoko wa benki ya Exim, Stanley Kafu alisema, “Mwaka huu benki ya Exim imefikia hatua muhimu sana. Tunasheherekea miaka 20 ya uvumbuzi na kujitolea kwa jamii. Kwa miaka mingi benki ya Exim imewekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya afya, mazingira na elimu nchini,

“Tunatambua juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya hivyo basi tumejitolea mwaka huu mzima kuwekeza katika hospitali za serikali katika maeneo mbalimbali nchini.”

Nae mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Satano Mahenge alipongeza Exim Bank Tanzania kwa ahadi yake ya kukabiliana na upungufu wa vitanda kwenye hospitali ambao unakabiliwa na taifa na kuleta juhudi zake kwa hospitali ya rufaa ya Dodoma.

Afisa wa matibabu wa Hospitali ya rufaa, Dodoma alisema, “Upungufu wa vitanda katika mahospitali ni changamoto kubwa. Msaada huu kutoka benki ya Exim wa hivi vitanda 40 na magodoro utasaidia sana katika kupunguza changamoto hii.”

Read 37 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli