We have 142 guests and no members online

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA BANDARINI DAR

Posted On Thursday, 30 November 2017 06:00 Written by
Rate this item
(0 votes)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kumkamata Wakala wa Kampuni ya Wallmark anayefahamika kwa jina la Samwel pamoja na Mfanyabiashara anayefahamika kwa jina la Bahman kutoka Kampuni ya NAS, kwa kosa la kutaka kutoa Bandarini magari makubwa 44 aina ya Semi tela bila ya kulipa kodi kwa kutumia jina la Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo leo Novemba 29, 2017 alipofanya ziara ya kushtukiza Bandarini jijini Dar es Salaam, baada ya kupata taarifa za mfanyabiashara huyo aliyetaka kutorosha  magari hayo yanayodaiwa kuingizwa nchini tangu mwaka 2015 kutoka nchini Uturuki.

“Mtu asije hapa aseme amepewa kibali na Rais Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia au Waziri Mkuu cha kuruhusu kutoa mzigo wake bila kufuata taratibu, akija mtu na taarifa hizo akamatwe mara moja na achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria,” alisema Waziri Mkuu.

Bahman wa kampuni ya NAS anadaiwa kutaka msamaha wa kodi kwa kuidanganya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) kuwa amewasiliana na Waziri Mkuu, na kwamba TPA wasipotekeleza agizo hilo watapata matatizo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa ameitaka TPA kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kutowasikiliza wafanyabiashara wanaotaka kukwepa kodi kwa madai ya kupewa vibali vya msamaha wa kodi kutoka viongozi wa juu serikalini.

Read 57 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji