We have 151 guests and no members online

“WANAUME TUMEKUWA WAGUMU SANA KUPIMA UKIMWI”- DKT. NDUGULILE

Posted On Saturday, 02 December 2017 13:22 Written by
Rate this item
(0 votes)

Wanaume nchini wamesisitizwa kuwa kipaumbele katika kupima Maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) ili kusaidia juhudi za Serikali katika kupambana na vita dhidi ya maambukizo ya ukimwi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa Kiunzi kazi wa Kutoa cheti kwa maeneo ya kufanyia vipimo vya VVU katika vituo vya kutolea huduma za afya.

“Wanaume tumekuwa wagumu sana katika kupima maambukizi ya virusi vya ukimwi na tukikutwa tuna maambukizi tunatakiwa tuanze kutumia dawa za kufubaza  kuliko kuwasubiri wenza wetu kwenda kupima na sisi ndo tupate majibu yetu kupitia wao,” alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kuhakikisha inapamabana na UKIMWI  wameweka taratibu ya kila mwananchi anayepima maambukizi ya Ukimwi na akagundulika kuwa na virusi hivyo anaanza dawa za kufubaisha mara moja.

Kwa mujibu wake Dkt. Ndugulile amesema kuwa mpaka kufikia 2020 Serikali inataka kufikia malengo ya kimkakati ya 90 90 90 ambayo 90 ya kwanza inamaanisha watu wapime VVU  kufikia asilimia 90, 90 ya pili inamaanisha wanaopima VVU kama wana maambukizi waanze kutumia dawa za kufubaza na 90 ya tatu inamaanisha wenye VVU wawe wamefubaza ugonjwa huo.

Aidha Dkt. Ndugulile ametoa rai kwa Watanzania wote kuchangia mfuko wa Udhamini wa kupamabana na Maambukizi ya Ukimwi kwa kupitia namba 0684909090 ili mradi kuweza kuongeza rasirimali fedha zitakazosaidia kwenye mapambano hayo.

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya ukimwi Duniani ambayo huadhimishwa Decemba 1 kila mwaka watu wote wajitokeze kupima VVU.

NA WAMJW, Dar es Salaam

Read 24 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu