We have 131 guests and no members online

WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA WAJIBU AKAUNTI YA NMB KUWAWEKEA WATOTO AKIBA

Posted On Tuesday, 05 December 2017 16:34 Written by
Rate this item
(0 votes)

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka wananchi kuwa na utaratibu wa kuwawekea watoto wao akiba ya fedha katika akaunti ya Wajibu ya benki ya NMB, kwa ajili ya matumizi ya baadae pindi zitakapohitajika.

Waziri Ummy aliyasema hayo wakati akizindua kampeni ya uhamasishaji wa elimu ya utunzaji wa fedha (Jifunze, Jipange, Wajibika) iliyoanzishwa na benki ya NMB.

Alisema wazazi na walezi wengi wamekuwa wakitumia pesa nyingi katika mambo ambayo hayana umuhimu mkubwa lakini wanasahau kuwa ni muhimu sana kuweka akiba kwa ajili ya watoto ambazo zitawasaidia kwa shughuli mbalimbali pindi watakapokua ikiwepo kulipia gharama za masomo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wa elimu ya utunzaji wa fedha (Jifunze, Jipange, Wajibika) iliyoanzishwa na benki ya NMB.

“Jambo kubwa nimefurahi NMB mmeamua kwenda kufunza watoto WAJIBIKA, tatizo Watanzania kwenye matumizi yetu hayana kipaumbele, Mtanzania kitchen party atachanga pesa nyingi sana lakini hawawawekei watoto akiba benki,

“Zaidi ya nusu ya Watanzania ni watoto, tunaweza kuona hii hela ni ndogo sana lakini ina umuhimu mkubwa katika kujenga uchumi, mfano tuwawekee 50,000 tutapata bilioni 500 ni pesa nyingi sana. Uchumi mkubwa inajenga kutoka uchumi mdogo, itaweza kusaidia kujenga uchumi wa serikali lakini pia kuwawekea akiba ya baadae,” alisema Waziri Ummy na kuongeza.

“Ujumbe wangu kwa Watanzania hela ambayo unaitumia kwa matumizi yasiyo ya lazima tenga angalau asilimia 5 kwa ajili ya mtoto wako. Kesho haianzi kesho, kesho inaanza leo na ili kuhakikisha kesho inaanza vizuri lazima kuweka akiba leo.”

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB, Ineke Bussemaker akizungumza katikahafla ya uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wa elimu ya utunzaji wa fedha (Jifunze, Jipange, Wajibika) iliyoanzishwa na benki ya NMB.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB, Ineke Bussemaker alisema NMB inatambua ni muhimu kwa watoto kujua umuhimu wa kujiwekea akiba hivyo ilianzisha kampeni hiyo ili kusaidia watoto kupata elimu ambayo wanaamini kwa kuwaelimisha watoto, itasaidia kwa miaka ijayo kuwa na kizazi ambacho kitakuwa kinaweka akiba.

“Ukianza na mtoto unaweza kusaidia elimu lakini pia jamii kupata elimu kuhusu umuhimu wa kuweka akiba ya fedha na wanapokua wanaweza kuitumia. NMB inajivunia kuanzisha akaunti kwa ajili ya watoto ili waanze kutunza pesa, hata kama ni kidogo wanaweza kuweka na wanaweza kuitoa muda wowote,” alisema Bussemaker.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB, Ineke Bussemaker wakitoa zawadi ya madaftari kwa baadhi ya wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wa elimu ya utunzaji wa fedha (Jifunze, Jipange, Wajibika) iliyoanzishwa na benki ya NMB.

Read 95 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart