We have 415 guests and no members online

BENKI YA EXIM YATOA MSAADA WA VITANDA NA MAGODORO KWA HOSPITALI YA MOUNT MERU

Posted On Monday, 18 December 2017 21:52 Written by
Rate this item
(0 votes)

Benki ya Exim Tanzania imekabidhi vitanda na magodoro 40 kwa Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru iliyoko mkoani Arusha, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa “miaka 20 ya kujali jamii” wenye lengo la kusaidia jamii.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Idara ya Masoko wa benki ya Exim, Bwana Stanley Kafu alisema, “Mwaka huu benki ya Exim imefikia hatua muhimu sana. Tunasheherekea miaka 20 ya uvumbuzi na kujitolea kwa jamii.

“Kwa miaka mingi benki ya Exim imewekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya afya, mazingira na elimu nchini. Tunatambua juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya hivyo basi tumejitolea mwaka huu mzima kuwekeza katika hospitali za serikali katika maeneo mbalimbali nchini.”

Afisa wa Matibabu wa Hospitali ya Mkoa Arusha Dkt. Vivian Wonanji alipongeza benki ya Exim Tanzania kwa kusaidia kukabiliana na upungufu wa vitanda kwenye hospitali hiyo ambayo inahudumia wagonjwa wengi kutoka mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania.

“Upungufu wa vitanda katika mahospitali ni changamoto kubwa. Msaada huu kutoka benki ya Exim wa hivi vitanda 40 na magodoro utasaidia sana katika kupunguza changamoto hii.” alisema Dkt. Wonanji.

Benki ya Exim Tanzania iliadhimisha miaka 20 ya huduma, mwezi wa Agosti mwaka huu, kwa kuzindua mradi wa mwaka mzima unaoitwa “miaka 20 ya kujali jamii” ambao benki hiyo itawekeza katika sekta ya afya Tanzania. Mradi huo unalenga kusaidia upungufu wa vitanda katika hospitali nchini ambapo benki ya Exim itatoa magodoro and vitanda 500 katika hospitali za serikali katika mikoa 13 nchini.

Hospitali ya Mount Meru imekuwa hospitali ya tano kupokea msaada huo, baada ya Hospitali ya Rufaa Dodoma, hospitali ya Rufaa Ligula ya Mtwara, Hospitali ya Mnazi Mmoja ya Unguja, Zanzibar na Hospitali ya Rufaa Temeke, Dar es Salaam

Read 46 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart