We have 411 guests and no members online

MAPENDEKEZO YA MUSWADA WA KUTOA TAARIFA YAFIKA PAZURI

Posted On Tuesday, 19 December 2017 11:36 Written by
Rate this item
(0 votes)

Imeelezwa kuwa kutungwa kwa sheria ya kulinda taarifa binafsi kutapunguza uhalifu unaohatarisha amani na kuongeza usalama wa mtu, jamii, nchi na dunia kwa ujumla.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo, amesema hayo katika kikao cha wadau cha kupitia mapendekezo ya kutungwa kwa sheria ya kulinda taarifa binafsi na kusisitiza umuhimu wa kujielimisha kabla ya kusambaza taarifa.

“Ni muhimu kwa jamii kuelewa haki ya faragha ya mtumiaji wa mawasiliano na namna ya kushughulikia taarifa katika ukusanyaji, usambazaji, uchakataji na uhifadhi ili kuepuka kutenda uhalifu” amesema Dkt. Sasabo.

Dkt. Sasabo amezungumzia umuhimu wa jamii kuzingatia sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 na sheria ya miamala ya kielektroniki ya mwaka 2015 ili kuepuka makosa yasiyo yalazima na kuepuka usambazaji wa taarifa binafsi za watumiaji wa mawasiliano usiouwiana na maadili na wenye nia ovu.

“Ni vema jamii ikajua mitandao haina mipaka, hivyo ni muhimu kuwa na muongozo utakaosimamia haki za watumiaji na kulinda taarifa binafsi”, amesisitiza Dkt. Sasabo.

Naye, Afisa Sheria wa Sekta ya Mawasiliano, Bi. Eunice Masigati, amesema mabadiliko ya sayansi na teknolojia yamechangia ongezeko kubwa la makosa katika mawasiliano ya simu na intaneti hivyo uwepo wa sheria inayosimamia taarifa binafsi utapunguza changamoto za kimtandao na kuongeza haki ya faragha.

Dkt. Sasabo, alikuwa katika kikao kazi cha wadau kukusanya maoni ya mapendekezo ya kutungwa sheria ya kulinda taarifa za watumiaji ili kupunguza uhalifu na kuhakikisha usalama wa taarifa binafsi.

Na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Read 43 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart