We have 400 guests and no members online

JESHI LA POLISI LAZUNGUMZIA KUPOTEA KWA MWANDISHI AZORI, BEN SAANANE NA LISSU

Posted On Thursday, 21 December 2017 05:51 Written by
Rate this item
(0 votes)

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), CP Robert Boaz amezungumzia kuhusu tukio la kupotea kwa Mwandishi wa gazeti la kila siku la Mwananchi Azory Gwanda, Mwanaharakati Ben Rabiu Saanane na tukio la kushambuliwa na risasi Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu.

CP Boaz akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya hali ya usalama nchini, ameeleza kuwa, Jeshi la Polisi limepokea taarifa za kupotea kwa Mwandishi Azory na kwamba limechukua hatua na zipo taratibu za kiupelelezi zinazoendelea na kuwataka watu kuwa na subira.

Kuhusu kupotea Ben Saanane, CP Boaz amesema Jeshi la Polisi haliwezi kusema kila hatua za kiupelelezi kuhusu tukio hilo kwa kuwa hairuhusiwi kisheria na taratibu za kiupelelezi, lakini amesema upelelezi unaendelea na kutoa rai kwa wananchi wenye taarifa sahihi kuzitoa ili kusaidia Polisi kukamilisha upelelezi.

Vile vile, CP Boaz amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuchukua hatua zenye kuwezesha upatikanaji wa watu waliohusika na tukio la kushambuliwa na risasi Tundu Lissu.

Tukio la kupotea Mwandishi Azory linadaiwa kutokea Novemba 21, wakati tukio la kushambuliwa na risasi Tundu Lissu lilitokea Septemba 7 mwaka huu, huku taarifa za kupotea Mwanaharakati Ben Saanane zilianza kusambaa Novemba 18 mwaka 2016.

Na Regina Mkonde-Dewjiblog

Read 105 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart