We have 413 guests and no members online

Wabunge nchini Uganda kupigia kura mswada wa kurekebisha Katiba

Posted On Thursday, 21 December 2017 05:56 Written by
Rate this item
(0 votes)

media

Bunge la Uganda

Wabunge nchini Uganda kwa siku ya tatu wanajadili mswada tata wa kuibadilisha Katiba, kuondoa kifungu cha sheria kinachozuia mtu aliye una umri wa miaka 75 kuwania urais nchini humo.

Mswada huo unatarajiwa kupigiwa kura siku ya Jumatano, huku wabunge wa chama tawala NRM wakitarajiwa kuupitisha.

Hata hivyo, wabunge wa upinzani ambao ni wachache, wamesema kwa kauli moja kuwa watapiga kura ya hapana.

Msimamo huu, umeonekana kuwavutia baadhi ya wabunge wa NRM ambao wamesema hawaungi mkono mabadiliko ya katiba baada ya kushauriana

Mbali na marekebisho hayo, baadhi ya wabunge pia wanataka mihula ya uongozi kurejeshwa katika katiba ya nchi hiyo.

Mjadala huu ulioanza siku ya Jumatatu umekumbwa na mvutano kati ya wabunhge wa pande zote mbili lakini pia wasiwasi wa kuwepo kwa maafisa wa usalama katika majengo ya bunge.

Siku ya Jumanne, vikao vya bunge viliahirishwa kwa muda baada ya kuwepo kwa madia ya wanajeshi kuvamia majengo ya bunge.

Wabunge wa upinzani wanasema serikali inatumia wanajeshi kwa lengo la kuleta uoga katika vikao vya bunge ili kupitisha mswada huo kwa nguvu.

Iwapo mswada huo utapitishwa, rais Yoweri Museveni ambaye ameongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 30, atawania tena urais mwaka 2021 akiwa na miaka 76.

Read 58 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart