We have 196 guests and no members online

POLISI YAIMARISHA ULINZI MKOANI IRINGA KABLA YA KRISMASI

Posted On Sunday, 24 December 2017 13:59 Written by
Rate this item
(0 votes)

Jeshi la Polisi limesema limeimarisha ulinzi kuelekea sikukuu za Krismasi na mwaka mpya ili kudhibiti vitendo vya uharifu pamoja na kupiga marufuku uchomaji wa matairi barabarani.

Akizungunza jana na Nipashe Jumapili, kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Iringa, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Julius Mjengi alisema jeshi la polisi katika kipindi cha sikukuu kuna watu wanajipanga kufanya uhalifu hivyo jeshi la polisi litafanya doria za kutosha katika wilaya za iringa, kilolo na mufindi.

Alisema kuwa wataimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali zikiwemo nyumba za ibada na kuwataka waumini wa kikristo wote kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa kristo mfalme bila hofu.

RPC Mjengi alisema madereva watakaondesha vyombo vya moto na kubainika wametumia vilevi watachukuliwa hatua kwani nia yao nakutaka kusababisha ajali ama kwa kudondodoka wao wenyewe au kugonga watembea kwa miguu.

Aidha alisema wazazi wanatakiwa kufanya ulinzi kwa watoto wao kutokana na watoto kupotea katika siku za sikukuu na kusababisha vituo vya polisi kuwepo kwa watoto hao.

Hata hivyo amesema wananchi watoe ushirikiano kwa jeshi la polisi pale wanapohisi kuna watu wanaashiria kufanya uhalifu.

Alisema jeshi hilo limejipanga kikamilifu kupambana na vitendo vyovyote vinavyoashiria uvunjifu waamanina sheria na kuwaomba wananchi kusherekea siku kuu hizo za krismasi na mwaka mpya.

Pia alisema kuwa uchomaji wa matairi barabarani kunapelekea kuharibu miundombinu ya barabara iliyojenjwa kwa gharama kubwa na kusababisha ajali baada ya miundombinu kuharibiwa.

Jeshi la Polisi mkoani iringa, linatoa tahadhari kwa wananchi, kuwa makini katika suala zima la ulinzi na usalama wa maisha na mali zao.

Uzoefu unaonyesha kwamba, katika kipindi kama hiki cha sikukuu kuna baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vya uhalifu. 

Hata hivyo, Jeshi la Polisi katika mkoa wa iringa na wilaya zake zote limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyojitokeza na pale vitakapoonyesha dalili ya kujitokeza viweze kudhibitiwa kwa haraka.

Na Friday Simbaya, Iringa

Read 46 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli