We have 418 guests and no members online

VIONGOZI WA UMMA WATAKIWA KUKABIDHI ORODHA YA MALI ZAO KABLA YA DESEMBA 31

Posted On Thursday, 28 December 2017 04:10 Written by
Rate this item
(0 votes)

 Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati alipowawataka Viongozi wote wa umma nchini kuorodhesha mali zao kisha kukabidhi kwa Sekretarieti kabla ya Desemba 31 mwaka huu Kulia ni Afisa Sheria Mkuu wa Sekretarieti hiyo Bw. Filotheus Manula.Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela katikati akikaribishwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Rodney Thadeus ili kuzungumza na waandishi wa habari, wa pili kutoka kulia ni Aisa Sheria Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Filotheus Manula na kushoto ni Ofisa wa Sekretarieti hiyo Bw. Waziri Kipacha


VIONGOZI wote wa umma nchini wametakiwa kuorodhesha mali zao tena kwa usahihi na kisha kukabidhi kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kabla ya Desemba 31 mwaka huu. 

Wamesisitiza kufanya hivyo ni utaratibu ambao upo kwa mujibu wa sheria ,hivyo lazima watekeleze kwa wakati na watakaoshindwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

 Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela wakati akitangza tarehe ya mwisho kwa viongozi wa umma kukabidhi tamko la mali zao ambayo ni Desemba 31 mwaka huu. 

“Kila kiongozi wa umma ajaze tamko hilo kwa kuorodhesha mali zake, mwenza wake na watoto wake walio na umri chini ya miaka 18,”amesema. Amefafanua viongozi wanaotakiwa kuorodhesha mali zao na kisha kukabidhi Sekretarieti ya Maadili ni wale wa kuteuliwa na kuchaguliwa. 

“Pia ujazaji wa tamko hilo kisheria linawahusisha hata viongozi waliostaafu na wale wanaoelekea kustaafu,”amesisitiza. Ameongeza viongozi ambao wanastaafu wakati wanaingia waliorodhesha mali zao, hivyo wanapostaafu ni lazima waoredheshe ili ifahamike wanatoka wakiwa na mali kiasi gani. 

“Hivyo ni muhimu kila kiongozi kujaza hilo tamko na tunachokifanya sisi ni kukumbusha tu.Fomu za tamko zipo kwenye tovuti ya sekretarieti ya maadili. “Huko nyuma tulikuwa tunawatafuta viongozi na kuwapa matamko wajaze lakini sasa ni lazima wao kuchukua na kujaza na jukumu letu ni kupokea na kisha kuchambua tamko la kila kiongozi,”amesema Jaji mstaafu Nsekela. 

Amesema anaamini viongozi wanafahamu wajibu wao,hivyo wafanye haraka iwezekanavyo na hasa kwa kuzingatia muda uliobakia ni mchache. Alipoulizwa ni viongozi wangapi wamejaza fomu hadi sasa,Jaji mstaafu Nsekela amesema hana takwimu sahihi lakini baada ya muda ulioapngwa kumaliza watatoa taarifa sahihi huku akieleza yeye tayari ameorodhesha mali zake kwenye tamko na kukabidhi tena kwa Rais. 

Kuhusu viongozi wanaostaafu ambao wamejaza tamko hilo amesema nao bado lakini katika eneo hilo kuna changamoto yake kidogo kwani viongozi wanapostaafu inakuwa ngumu kuwapata lakini nao watambue wanatakiwa kujaza tamko kwa mujibu wa sheria. 

Kwa upande wake, Ofisa Sheria Mkuu wa Sekretarieti ya Mmaadili Bw. Filotheus Manula ameongeza ujazaji wa tamko la mali kwa viongozi wa umma ni takwa la kikatiba na kuna adhabu kwa wasiofuata. 

Ametaja adhabu hizo ni kuonywa, kushushwa cheo, kusimamishwa kazi na wakati mwingine kufukuzwa kazi. 

Read 60 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart