We have 396 guests and no members online

WANANCHI WAMIMINIKA KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA KAHAMA

Posted On Sunday, 31 December 2017 12:40 Written by
Rate this item
(0 votes)

Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa akimsajili mmoja wa Wananchi wa Kata ya Kahama Mjini aliyejitokeza kusajiliwa wakati zoezi la usajili likiendelea kwenye Kata hiyo.Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa 16 ya Tanzania ambayo zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa linaendelea huku mamia ya wananchi wakionekana kuhamasika na zoezi hilo kwa kujitokeza kwa wingi kwenye vituo ambavyo usajili umekuwa ukiendelea.

Akizungumzia zoezi hilo Afisa Usajili wa Wilaya ya Kahama bwana Ibrahim amesema mwitikio mkubwa wa watu katika vituo vya usajili ni kiashiria kwamba uelewa wa wananchi ni mkubwa na kwamba wanatambua vitakavyowasaidia katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Akizungumzia gharama za zoezi afisa huyo ameeleza zoezi ni BURE na kwamba mwananchi hapaswi kutozwa kiasi chochote cha fedha zaidi ya kufika na nakala (photocopy) za nyaraka/viambatanisho muhimu vya kuweza kumtambulisha uraia wake, umri na makazi. Mfano wa nyaraka hizo ni; Kadi ya mpiga kura, cheti cha kuzaliwa, leseni ya udereva, ID ya Mzanzibar mkazi, TIN, Pasi ya kusafiria, vyeti vya elimu nk.

Mbali na Shinyanya mikoa mingine ambayo NIDA inaendesha zoezi ni Iringa, Mara, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Songwe, Njombe, Singida, Manyara, Mwanza, Simiyu, Mara, Geita, Lindi, Mtwara na Ruvuma

Read 58 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart