We have 403 guests and no members online

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA BABU SEYA NA WATOTO WAKE

Posted On Tuesday, 02 January 2018 19:54 Written by
Rate this item
(0 votes)

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na Mwanamuziki Nguza Viking na watoto wake waliofika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumshukuru kwa kupatiwa msamaha wa kuachiwa huru kwake Nguza Viking (Babu Seya) na mwanae Papii Nguza (Papii Kocha) waliokuwa wakitumikia adhabu ya kifungo cha maisha jela.

Mzee Nguza Vicking (Babu Seya) akiwa na watoto wake Papii Nguza (Papii Kocha), Francis Nguza pamoja na Michael Nguza walipomtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwaajili ya kumshukuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mzee Nguza Vicking (Babu Seya) akifurahi na watoto wake Papii Nguza (Papii Kocha), Francis Nguza pamoja na Michael Nguza walipomtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli kwaajili ya kumshukuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mzee Nguza Vicking (Babu Seya) aliyeambatana na familia yake kwaajili ya kumshukuru Mheshimiwa Rais Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mzee Nguza Vicking (Babu Seya) pamoja na familia yake walipomtembelea kwaajili ya kumshukuru Mheshimiwa Rais Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na Mzee Nguza Vicking (Babu Seya) pamoja na familia yake wakiomba dua walipomtembelea kwaajili ya kumshukuru Mheshimiwa Rais Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mzee Nguza Vicking (Babu Seya) pamoja na familia yake walipomtembelea kwaajili ya kumshukuru Mheshimiwa Rais Ikulu Jijini Dar es Salaam

Read 52 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart