We have 194 guests and no members online

“MAENDELEO HAYANA MIPAKA YA VYAMA”- NAIBU WAZIRI WA KILIMO

Posted On Wednesday, 03 January 2018 06:56 Written by
Rate this item
(0 votes)

Maendeleo ni mchakato wa kujenga jamii endelevu, yenye kujiamini, kujituma na uwezo wa kushiriki, kwa misingi ya usawa na kuheshimiana, katika kubuni, kuandaa na kutekeleza mipango ya kujiletea “maendeleo” na kutumia matokeo ya kazi zao.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mary Mwanjelwa ameyasema hayo Jana 2 Januari 2018 wakati akizungumza na wananchi na mafundi wanaojenga majengo ya Shule ya Sekondari Iyera ili kutatua changamoto ya kuwa na vyumba vingi vya madarasa kwa ajili ya kuhimili wingi wa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu.

Amewasisitiza mafundi hao kujenga madarasa hayo kwa haraka na viwango vya hali ya juu kwani shule zinatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni huku shule hiyo ikiwa na upungufu wa vyumba vinne vya madarasa.

Mwanjelwa alisema kuwa tangu serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutangaza utoaji elimu bure kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi sekondari kumekuwa na ongezeko kubwa la wananfunzi wanaojiunga na masomo ikiwa ni pamoja na kurejea shuleni kwa wananafunzi waliokata tamaa ya kuendelea na masomo.

Alisifu juhudi za Uongozi wa Wilaya ya Mbeya kwa kushirikiana kwa pamoja na wananchi katika shughuli za maendeleo huku akiipongeza Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa kufanya vyema na hatimaye kuongoza kwa ufaulu wa wanafunzi dhidi ya Halmashauri zingine za Mkoa wa Mbeya.

Sambamba na hayo pia Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa ameongeza nguvu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule hiyo ya Sekondari Iyera kwa kuchangia mifuko 20 ya saruji.

Na Mathias Canal, Mbeya

Read 25 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi