We have 217 guests and no members online

Simulizi Za Kusisimua Za Kombe La Dunia... Kocha Wa Brazil Aliyefanya Kituko Cha Kihistoria..

Posted On Wednesday, 03 January 2018 08:47 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image may contain: 1 person

Ndugu zangu,

Leo nitasimulia fainali za tatu za Kombe la Dunia za mwaka 1938 nchini Ufaransa. FIFA ilitumia ‘hila’ kuifanya Ufaransa kuwa mwenyeji wa fainali za mwaka 1938.

Ikumbukwe , kuwa Ufaransa ndiko alikotoka Rais wa FIFA wa wakati huo, Bw. Jules Rimet. Mara tu FIFA ilipotoa uamuzi wa kuzipeleka fainali hizo Ufaransa, hapo hapo Argentina wakatangaza kususia fainali hizo.

Nchi nyingine kadhaa za Marekani ya Kusini ziliungana na Argentina, lakini, Brazil na Cuba wao waliamua kushiriki.

Enyi wapenzi wenzangu wa kandanda, ni vema tukakumbushana kuwa fainali za mwaka 1938 zilichezwa huku buti za askari wa fashisti Hitler wa Ujerumani na mwenzake Benito Mussolini wa Italia zikianza kutikisa ardhi ya dunia. Wingu la Vita vya Pili vya Dunia lilianza kutanda duniani.

Mathalan, wakati fainali hizo zikichezwa, vikosi vya Hitler vilishaingia kwa gwaride nchini Austria. Mussolini naye alishaamuru vikosi vyake kuitwaa milima ya Abbessinia kule Ethiopia. Katika hili, inaandikwa, kuwa hata askari wa Kihehe waliopigana upande wa Hitler walikuwepo pia Abbysinia.

Wakati huo huo, ndani ya Hispania kulikuwa na mlipuko wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Nchi ya Austria, ambayo ilishafuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia kule Ufaransa, ililazimika kujitoa kutokana na nchi hiyo kuvamiwa na vikosi vya Hitler.

Badala yake, wachezaji wao nyota wanne walikuja kuichezea timu ya Ujerumani kwenye fainali hizo.

Kwa ufupi, hali ya dunia ilikuwa tete na Vita Vya Pili vya Dunia vilikuwa vinakaribia kwa kasi.

Tukirudi kwenye fainali zenyewe, mechi iliyokuwa na msisimko wa kipekee kule Ufaransa ni ile kati ya Brazil na Poland. Ni kwenye raundi ya kwanza ya mtoano. Dakika 90 za mchezo zilipomalizika, timu zilitoka uwanjani kwa sare ya 4-4! Brazil iliibuka na ushindi wa 6-5. Ni baada ya dakika 30 za nyongeza.

Leonidas ( Pichani) ndiye alikuwa mshambuliaji hatari wa Brazil wa wakati huo. Huyu alikuwa na asili ya Afrika na aliitwa pia ”Dhahabu Nyeusi” kama jina la utani. Katika mechi hiyo na Poland, Leonidas alipachika mabao matatu peke yake kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo. Kwanini inasemwa kuwa kocha wa Brazil alifanya kituko cha historia kuhusiana na Leonidas? Itaendelea kesho..

Maggid,

Read 80 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli