We have 476 guests and no members online

RC SIMIYU AMSIMAMISHA KAZI MWENYEKITI NA WAJUMBE WA SERIKALI YA KIJIJI

Posted On Tuesday, 09 January 2018 11:57 Written by
Rate this item
(0 votes)

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amemsimamisha kazi kwa muda wa mwezi mmoja Mwenyekiti wa Kijiji cha Lamadi Wilayani Busega, Nzala Hezron pamoja na Wajumbe wa Serikali ya Kijiji hicho, ili kupisha uchunguzi kufuatia tuhuma mbalimbali zinazowakabili.

Uamuzi huo umekuja kufuatia malalamiko yaliyotolewa na wananchi wa Lamadi dhidi ya Mwenyeiti huyo kwa Mkuu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana Lamadi, kuhusu tuhuma mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za michango ya wananchi katika Ujenzi wa Shule ya Sekondari Lukungu pamoja na kutosoma mapato na matumizi ya fedha za michango mbalimbali ya wananchi.

“Ili tuweze kutenda haki ya uchunguzi na ukaguzi tumeona ni busara Mwenyekiti asiwe Ofisini na wajumbe wanaounda Serikali ya Kijiji wasiwe ofisini ili uchunguzi na ukaguzi wa akaunti uweze kufanyika kwa haki,” alisema Mtaka.

Mtaka amesema Mkaguzi wa Ndani kutoka katika Ofisi yake atakayeshirikiana na Mkaguzi wa ndani wa Wilaya ya Busega kufanya ukaguzi katika Akaunti ya Shule kujua namna fedha zilizochangwa na wananchi na zilizotolewa na Halmashauri zilivyofanya kazi ya Ujenzi wa Vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika Shule ya Sekondari Lukungu.

Na StellaKalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu

Read 49 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart