We have 140 guests and no members online

Simulizi Za Kombe La Dunia: Nchi Mbili Jirani Ziliingia Vitani Kwa Matokeo Ya Uwanjani

Posted On Sunday, 21 January 2018 20:51 Written by
Rate this item
(0 votes)


- Uwanjani 3-1, Vitani Sare

Ndugu zangu,

Kandanda ni zaidi ya mchezo, ni siasa pia. Kuna marais waliobaki madarakani au waliong’oka madarakani kutokana na matokeo mabaya au mazuri ya timu zao za taifa. Soka imeleta uhasama baina ya mtu na mtu, kabila na kabila na hata taifa moja dhidi ya taifa jingine.

Katika historia tunasoma kuwa mchezo huu wa kandanda umewahi kusababisha vita baina ya nchi mbili jirani kule Marekani ya Kusini, ni Honduras na El Salvador.

Ilikuwa ni mwaka 1969 wakati wa mechi za mataifa kuwania tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1970. Katika mchezo wa kwanza Honduras walikuwa wenyeji.

El Salvador walifika Honduras na wakapata mapokezi baridi sana. Usiku wa kuamkia mechi, wakiwa kwenye hoteli 
waliyofikia, wachezaji wa El Salvador walifanyiwa fujo na wapenzi wa soka wa Honduras waliofika kwa wingi na kuizunguka hoteli yao.
Wakiwa nje ya hoteli waliofikia wageni, wapenzi wale walipiga kelele, waligonga masufuria kwa vyuma na walipiga honi za magari usiku kucha. Masikini, wachezaji wa El Salvador hawakupata nafasi ya kulala usiku mzima. Kulipokucha walionekana kuwa wachovu mno. Walishinda hotelini bila 
kupata nafasi ya kunyosha miguu kwa kutembea mitaani. Polisi waliwaambia wabaki humo humo hotelini kwa usalama wao.

Habari za timu ya taifa kufanyiwa hujuma hizi zilifika nyumbani 
El Salvador hata kabla ya mechi kuanza siku hiyo. Jambo hili liliamsha hisia za utaifa, hasira na chuki kubwa kwa watu wa El Salvador dhidi ya jirani zao Honduras. Muda wa mechi uliwadia. Mechi ilichezwa kwenye uwanja wa Tagucigalpa. Pamoja na vurugu walizofanyiwa na kushindwa kulala usiku, vijana wale wa El Salvador walipigana kishujaa uwanjani kutetea hadhi na 
heshima ya taifa lao. Zikiwa zimebaki dakika chache mpira kwisha, timu mwenyeji , Honduras walipachika bao la ushindi. Honduras waliibuka washindi kwa bao 1-0.
Nyumbani El Salvador , msichana mmoja aliyekuwa akitazama pambano hilo kupitia luninga alifadhaishwa sana kuona nchi yao ikipoteza mchezo ule katika mazingira yale. Aliamua kujiua.

Kwa moyo wake wa uzalendo na uchungu kwa nchi yake, msichana yule alitajwa kuwa shujaa wa taifa. Mazishi yake 
yalikuwa ya kitaifa. Msafara wa mazishi uliwahusisha pia wachezaji wa timu ya taifa ya El Salvador.

Majuma mawili baadae ikafika siku ya mchezo wa marudiano. Safari hii El Salvador walikuwa wenyeji wa Honduras. Haikuwa mechi ya marudiano ya kawaida, ilikuwa ni mechi ya kulipiza kisasi.

Nini Kilitokea?

Itaendelea kesho.

Maggid.

Read 67 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart