We have 382 guests and no members online

KAMISHNA WA TUME YA MAADILI AWATAKA WADAU KUJADILI KANUNI MPYA ZA TUME HIYO.

Posted On Saturday, 27 January 2018 11:32 Written by
Rate this item
(0 votes)

Tokeo la picha la Harold Nsekela

Kamishna wa tume ya maadili jaji mstaafu Harold Nsekela amewataka wadau na viongozi kujadili kanuni mpya za maadili kwa kuangalia mgongano wa kimaslahi kwa viongozi wa umma hususani kutenganisha shughuli binafsi za kiongozi na wadhifa wake.

Amesema hayo wakati akiwasilisha rasimu ya sekeretarieti ya maadili kwa wadau na viongozi ili ijadiliwe na kuweka uelewa wa pamoja wa nini kinatakiwa katika kanuni zinazopendekezwa na kuyataja maeneo muhimu kwenye rasimu na kanuni za maadili zinazopendekezwa kuwa ni pamoja na:

  • Masuala ya Mgongano wa kimaslahi ambayo yanafafanuliwa kwenye sehemu ya tano ya rasimu hiyo.
  • Tamko la rasilimali na madeni linalotolewa ndani ya siku 30 tangu kupewa madaraka, na walau mwezi mmoja kabla ya kustaafu.
  • Uhakiki wa rasilimali na madeni ya viongozi wa umma ambao hufanywa walau mara moja kila mwaka mara baada ya kupokea tamko la rasilimali na madeni.
  • Kutangaza mali na madeni.

Aidha amesema kuwa sekretarieti imeona kuna haja ya kutengeneza kanuni itakayojumlisha masuala muhimu yanayofaa kwa ajili ya utendaji bora wa utekelezaji wa sharia ya maadili ya viongozi wa umma.

Lengo la kuwashirikisha wadau na viongozi katika kujadili rasimu hiyo, ilikuwa ni pamoja na uzoefu walionao katika kusimamia masuala ya utawala bora, baadhi yao wamekuwa wakishughulikia kwa vitendo masuala ya maadili katika taasisi zao na kuwasaidia viongozi wasijiingize katika mgongano wa maslahi, na tatu baadhi yao (wabunge) wamekuwa watunga sharia na wana uelewa namna ya sharia inavyotumika.

Read 47 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli