We have 340 guests and no members online

IGP SIMON SIRO ATOA SHUKURANI KWA VIONGOZI WA DINI.

Posted On Sunday, 28 January 2018 03:42 Written by
Rate this item
(0 votes)

Tokeo la picha la igp simon siro

Mkuu wa jeshi la polisi Tanzania IGP Simon Siro amesema jeshi la polisi limefanikiwa kuimarisha amani nchini kwa kuwakamata wahalifu huku baadhi yao wakikimbilia nje ya nchi hasa Msumbiji. IGP Siro alipokuwa akiongea na viongozi wa dini jijini Dar es Salaam, kuwajulisha hali ya utulivu iliyopo imechangiwa na mahusiano na uhirikiano ulioonyeshwa hasa kipindi cha changamoto kubwa kwenye maeneo ya Kibiti na Ikwilili.

Vilevile amesema jeshi la polisi Tanzania limefanya mawasiliano na IGP wa msumbiji ambaye yeye anasema wamewakamata vijana zaidi ya 60 wakiwa msituni, wengi wao wakiwa ni Watanzania.
Kwa upande wa changamoto iliyopo amesema wahalifu wengine wamekimbilia maeneo ya Msumbiji, na wanaweza wakarudi kufanya uhalifu.

Read 71 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli