We have 299 guests and no members online

JPM ASHIRIKI IBADA YA KUAGA MWILI WA JAJI KISANGA.

Posted On Sunday, 28 January 2018 16:08 Written by
Rate this item
(0 votes)

Tokeo la picha la RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MAZISHI YA JAJI KISANGA

Tokeo la picha la RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MAZISHI YA JAJI KISANGA

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Bi.Mama Janeth Magufuli, wameyaongoza mamia ya waombolezaji katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Jaji mstaafu Robert Kisanga ambaye alifariki Dunia mwezi January 23 mwaka huu.

Rais Magufuli amepokelewa na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma alipofika nyumbani kwa Marehemu Jaji Kisanga na kisha kuweka saini katika kitambu cha maombolezo na baadae kumfariji mjane wa marehemu Mama Maria Kisanga.

Akiwa na mke wake Mama Janeth, Rais Magufuli ameshiriki katika kufanya sala maalumu ya pamoja na familia ya marehemu Kisanga kwa ajili ya kumuombea marehemu huyo. Jaji Kisanga alifariki Dunia Januari 23 katika hospitali ya Regency alipokuwa akipatiwa matibabu.

Read 87 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu