We have 318 guests and no members online

"KAMA UTATAKA KUFILISIKA, JIHUSISHE NA UVUVI HARAMU" LUHAGA MPINA

Posted On Monday, 29 January 2018 04:50 Written by
Rate this item
(0 votes)

Picha inayohusiana

Waziri wa mifugo na uvuvu Luhaga Mpina amesema uvuvi haramu ni moja kati ya majanga yanayomaliza rasilimali za wananchi ambazo zingetumika kufanya shughuli nyingine kama uwasomesha watoto.

Waziri Mpina amesema hayo wakati akizungumza na wavuvi mkoani Mara katika oparesheni ya kutokomeza uvuvi haramu inayofanywa nchini kote, ambapo mpaka sasa zana haramu na nyavu zisizoruhusiwa kisheria mkoani Mara, ambazo thamani yake ni zaidi ya shilingi bilioni 4 zimeteketezwa.

Pia waziri Mpina amewaonya wote wanaojihusisha na kutengeneza, kuingiza na kuuza nyavu haramu kwamba sharia itachukuliwa dhidi yao. Kwa upande wao baadhi ya wavuvi na wakazi wa mkoa wa Mara wametoa malamiko yao kwa waziri Mpina kwamba maafisa uvuvi wanashindwa kutoa elimu juu ya kuepuka uvuvi haramu zaidi ya kuwanyang’anya mali na kuharibu mitumbwi yao.

Read 60 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli