We have 130 guests and no members online

WADAU WA HABARI KENYA WAKOSOA KUZIMWA KWA MITAMBO VITUO VYA TV.

Posted On Tuesday, 30 January 2018 12:07 Written by
Rate this item
(0 votes)

Tokeo la picha la kuzimwa vituo vya tv kenya

Mkurugenzi Mkuu wa Royal Media Services inayomiliki Televisheni ya Citizen TV, Waruru Wachira, amelaani hatua iliyochukuliwa na serikali kufunga mawasiliano katika vituo vya runinga na kusema kuwa binafsi hakutaarifiwa lolote kuhusu hatua hiyo iliyokuja ghafla ambayo pia imeathiri kituo chake cha Citizen TV. Katika hatua hiyo iliyoamuliwa na serikali vituo kadhaa vimeathirika ikiwa ni pamoja na kituo cha Citizen TV, KTN News na NTV.

Matangazo ya runinga hizo yalihamishiwa kwenye mtandao wa Youtube.

Sababu kubwa iliyofanya tume ya Mawasiliano nchini humo kuzima mitambo ya Televisheni ni kuzuia kuonekana kwa sherehe za kuapishwa kwa kiongozi wa muungano wa upinzani NASA Raila Odinga kuwa rais wa watu. Awali Siku ya Ijumaa wiki iliyopita, serikali ilishtumiwa kwa kutishia kufunga mitambo ya vituo ambavyo vingerusha matangazo ya moja kwa moja ya kuapishwa kwa Odinga moja, pamoja na kuvipokonya leseni vituo hivyo, tamko ambalo lililalamikiwa na jukwaa la Wahariri. Wadau wa Habari nchini humo wamelaani hatua ya serikali suala ambalo wamesema ni ukiukwaji wa haki za vyombo vya Habari nchini humo.

 

Read 56 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart