We have 129 guests and no members online

UNHCR LASEMA MAPIGANO DRC YAMEONGEZA ZAIDI WAKIMBIZI.

Posted On Wednesday, 31 January 2018 08:20 Written by
Rate this item
(0 votes)

 

Tokeo la picha la unhcr in drc

Shirika la Umoja wa Mataifa la UNHCR linaloshughulikia wakimbizi limesema mapigano yanayoendelea mashariki mwa DRC yameongeza wimbi la wakimbizi wanaoingia nchi jirani za Burundi, Tanzania na Uganda.

Huku mapigano dhidi ya makundi yenye silaha ya Mai Mai yakiendelea Kusini mwa Jimbo la Kivu nchini humo, maelfu ya watoto, wanawake na wanaume wameyaacha makazi yao.

Shirika hilo limesema takrinani wakimbizi 1200 wameingia nchini Tanzania, huku ikiaminika kwamba kuna wimbi kubwa zaidi la wakimbizi ambao wapo Kivu Kusini wakiwa katika hali mbaya ya kukosa chakula na makazi.

Kwa upande wake Bi Joan Allison ni naibu mwakilisha wa UNHCR nchini Tanzania amesema katika jumla ya wakimbizi 1200, wanaume ni 300 tu, na wanakuja nchini Tanzania kupitia ziwa Tanganyika kwa kutumia boti huku baadhi wakiwa katika hali mbaya ya kiafya.

Joan.Ameongeza kwa kusema, "Rasilimali ni chache kwa wakimbizi, mahitaji ni makubwa. Tunajitahidi kadri tunavyoweza lakini tunahitaji rasilimali zaidi iwapo hali itaendelea kuwa tete”.

Wimbi kubwa la wakimbizi limeelezwa kuongeza changamoto ya upatikanaji wa malazi, maji na hata huduma za choo, huku wengine wakiwa hawana jinsi zaidi ya kulala katika sehemu zilizo wazi.

Read 43 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart