We have 131 guests and no members online

WAZIRI KALEMANI AWAAGIZA VIONGOZI KIGOMA KUSIMAMIA MIRADI YA UMEME WA REA

Posted On Wednesday, 31 January 2018 09:13 Written by
Rate this item
(0 votes)

26994092_2017314731879806_1589958551452772932_n

Waziri wa Nishati wa Dkt. Medard Kalemani amewaagiza Viongozi wa wilaya za Kakonko na Kibondo pamoja na Meneja wa Shirika Umeme TANESCO kwenye wilaya hizo mkoani Kigoma kuhakikisha wanasimamia miradi ya umeme vijijini REA kwa awamu ya tatu katika maeneo yao ili kutimiza malengo ya serikali. Waziri Kalemani amesema hayo alipokuwa akizindua mradi wa Umeme Vijijini (REA) awamu ya tatu Mkoani Kigoma, ambapo uzinduzi huo umefanyika katika kijiji cha Mabamba wilayani Kibondo.

Aidha amesema serikali imetenga Shilingi bilioni 60 kwa kugharamia miradi ya umeme kwa Mkoa wa Kigoma ambapo shilingi bilioni 25 zimetengwa kwa wilaya za Kibondo na Kakonko na hivyo viongozi wa wilaya hizo wanapaswa kuwasimamia wakandarasi kuhakikisha wanafanya kazi kwa wakati.

Kwa upande wake Brigedia Generali Mstaafu Emmanuel Maganga mkuu wa mkoa wa Kigoma amemuhakikishia waziri Kalemani kuwa ofisi yake itasimamia miradi hiyo kwa karibu na kuwahimiza viongozi wa wilaya ya Kibondo kuwasimamia wakandarasi kwenye maeneo yao ili kutimiza malengo ya serikali ya kuwafikishia maendeleo wananchi.

Read 52 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart