We have 125 guests and no members online

KENYA; MWANAHARAKATI ATINGA MAHAKAMANI KUDAI SABABU KISHERIA ZA KUFUNGA VITUO VYA TV.

Posted On Thursday, 01 February 2018 08:31 Written by
Rate this item
(0 votes)

Tokeo la picha la Okiya Omtatah

Mwanaharakati nchini Kenya Okiya Omtatah ametinga mahakamani kupata mwafaka kisheria kuhusu kufungwa kwa vituo vitatu vya runginga nchini humo jambo ambalo ameliita ni kinyume cha katiba ya nchi. Katika madai yake ambayo yanatakiwa kusikilizwa leo Februari mosi, Bw. Omtatah amesema uamuzi wake wa kwenda mahakamani ni kutokana na uamuzi wa serikali kuvifungia vituo vya NTV, Citizen na  KTN News na kwamba uamuzi huo unakiuka kifungu namba 33 na 34 cha katiba ya nchi.

Madai ya mwanaharakati huyo yanaambatana na kuitaka serikali kulipa fidia kwa hasara ambazo vituo hivyo vilipata wakati matangazo yalipozimwa tarehe 30 Januari.

“Bila kutoa tahadhari, bila kutoa sababu yoyote, asubuhi ya tarehe 30 Januari 2018, mamlaka husika ilifunga mitambo ya kurusha matangazo kwenye vituo vya runinga,” Ameongeza.

Amesema kifungu cha kwanza cha sheria namba 33 inatoa mwanya kwa kila mtu uhuru wa kujieleza ikiwa ni pamoja na haki ya kutafuta, kutoa na kupokea mawazo au taarifa muhimu. Na hivyo haki ya wananchi kupata habari imeathiriwa kutokana na hatua hiyo.

Read 25 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart