We have 136 guests and no members online

KAMPUNI YA TTCL SASA YABADILISHWA NA KUWA SHIRIKA LA MAWASILIANO.

Posted On Thursday, 01 February 2018 09:09 Written by
Rate this item
(0 votes)

Tokeo la picha la prof mbarawa TTCL

Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Prof Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ametoa tamko rasmi la kuibadilisha  kampuni ya mawasiliano TTCL kutoka kampuni ya mawasiliano na sasa litakuwa Shirika la Mawasiliano la umma.

Waziri Mbarawa amesema uwepo wa sheria ya shirika la mawasiliano unatoa fursa ya kuboresha sekta ya mawasiliano kwa kuweka mazingira mazuri ya usimamizi wa miundombinu ya kimkakati, ikiwemo mkonga wa taifa wa mawasiliano, ‘data center’, na kuongeza kuwa kihistoria TTCL ina usalama wa nchi.

Aidha mabadiliko ya kuhama kutoka kampuni ya mawasiliano na kuwa shirika la mawasiliano, hayataathiri utoaji wa huduma mbalimbali za mawasiliano zilizokuwa zikitolewa na kampuni ya simu ya TTCL kwa wananchi, na kwamba huduma zote za kimawasiliano ikiwemo simu za mkononi, Internet na TTCL-Pesa  zitaendelea tena kwa kiwango cha ubora zaidi.

Read 41 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart