We have 301 guests and no members online

HOFU KWA WANAHABARI WA KENYA, WAHOFIA KUKAMATWA NA POLISI

Posted On Thursday, 01 February 2018 10:34 Written by
Rate this item
(0 votes)

 

Tokeo la picha la kenyan journalistsChanzo, DW.

Wanahabari watatu wa Kenya walilazimika kukesha katika chumba cha habari kwa kuhofia kukamatwa na polisi waliokuwa wameweka kambi nje ya majengo ya shirika la habari la habari la Nation. Mawakili wa wanahabari hao wamewasilisha maombi mahakamani ya kutaka hakikisho la uhuru wa wanahabari hao.

Kituo cha NTV wanachofanya kazi Linus Kaikai ambaye ni mhariri mkuu na mwenyekiti wa chama cha wahariri nchini Kenya, Larry Madowo na Ken Mijungu ni miongoni mwa vituo vitatu vya televisheni ambavyo vilifungiwa kuonesha matangazo yao na serikali baada ya kukiuka agizo la serikali la kutoonesha matangazo ya moja kwa moja ya hafla ya kujiapisha kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwa rais wa nchi. Madowo amesema hatua hiyo ya serikali ina ishara zote za utawala wa kidikteta.

Read 31 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli