We have 377 guests and no members online

TATIZO LA MAJI LINDI MJINI KUBAKI HISTORIA

Posted On Thursday, 01 February 2018 13:05 Written by
Rate this item
(0 votes)

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo amefanya ziara kutembelea mradi wa maji wa Ng’apa Mkoani Lindi wenye thamani ya Euro milioni 11.7 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Serikali.

Profesa Mkumbo amesema kuwa wananchi wa Lindi wanaanza kupata huduma ya maji leo Februari mosi huku kazi ndogondogo zilizobaki katika mradi huo zikiendelea kukamilishwa.

Akifafanua amesema kuwa mradi huu unatarajia kuzalisha kiasi cha lita milioni 7 za maji kwa siku kiasi ambacho kitakidhi mahitaji ya maji Lindi mjini kwa sasa na kuchochea ukuaji wa uchumi na uzalishaji, Aidha mahitaji ya maji ya mji huo ni kiasi cha lita milioni 5 kwa siku .

“Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Lindi (LUWASA) itafanya kazi ya ukarabati wa miundombinu iliyopo pamoja na kuongeza mtandao katika vitongoji ambavyo havina mtandao wa mabomba,” alisisitiza Profesa Mkumbo.

Aidha, Profesa Mkumbo ametoa wito kwa wananchi Mkoani Lindi kulinda miundombinu ya maji na kulipa ankara za maji waliyotumia ili huduma hiyo iwe endelevu na ichangie katika kuleta maendeleo.

Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imeweka mkazo katika kuimarisha huduma za jamii hasa zile zinazowagusa wananchi wanyonge ikiwemo upatikanaji wa maji safi na Salama kwa wananchi wake kote nchini hali inayochochea kasi yautekelezaji wa miradi ya maji katika Mikoa na Wilaya mbalimbali hapa nchini.

Mradi huo umetekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji ambapo mkandarasi ni Kampuni ya OIA ya nchini india.

Read 39 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli