We have 341 guests and no members online

NIGERIA; WATU WANNE WAUWAWA. KUNDI LA BOKO HARAM LADHANIWA KUTEKELEZA SHAMBULIO LA KIGAIDI.

Posted On Thursday, 01 February 2018 14:44 Written by
Rate this item
(0 votes)

Tokeo la picha la bobo haram attack

Takribani watu wanne wamepoteza maisha katika shambulio la kujitoa muhanga lililotokea kwenye kambi ya wakimbizi mjini Maiduguri Kaskazini mashariki mwa Nigeria ambapo kundi la Boko Haram linaaminika kuhusika na shambulio hilo.

Taarifa kutoka nchini humo zinaeleza mshambuliaji aliruka ukuta wa kambi wakimbizi ya Dolari na kulipua bomu baada ya kujicahnganya miognoni mwa wakimbizi kambini humo na kuwauwa watu wanne huku wengine 44 wakijeruhiwa baadhi wakielezwa kuwa katika hali mbaya.

Muda mfupi baada ya tukio hilo mshambuliaji mwingine wa kike alijilipua ingawa hata hivyo hakuna madhara yoyote yaliyoripotiwa.

Taarifa zinaeleza kuwa mwanamke mmoja aliejichanganya miongoni mwa watu kambini hapo, lakini baada ya kushukiwa, watu wote walimkimbia kabla ya mwanamke huyo kujilipua.

Mashambulizi hayo mawili yanakuja wakati makundi ya wapiganaji wajadi wakijiandaa kukabiliana na wapignaji wa kijihadi wa Boko Haram kuwaondoa katika msitu wa Sambisa.

Read 40 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli