We have 384 guests and no members online

MIKATABA YA MRADI WA MLIMANI CITY YAANZA KUZUNGUMZIWA BUNGENI.

Posted On Thursday, 01 February 2018 18:57 Written by
Rate this item
(0 votes)

 

Tokeo la picha la mlimani city

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imelitaka Bunge liazimie kumuomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi wa mchakato wa mikataba yote ya mradi wa Mlimani City. Naghenjwa Kaboyoka mwenyekiti wa PAC wakati akiwasilisha bungeni taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kamati hiyo leo Februari1, 2018, amesema kamati hiyo imebaini dosari katika mkataba wa uendeshaji wa mradi huo, kusababisha Serikali kukosa mapato.

Miongoni mwa dosari za mradi huo zilizotajwa ni paamoja na kukiukwa kwa sheria ya Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) inayotaka ili kibali cha uwekezaji kutolewa lazima mwekezaji alete ushahidi kuwa na mtaji wa kutosha. Eneo la Mlimani City lilikodishwa kwa kampuni ya Mlimani Holding Ltd, kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Katika siku za hivi karibuni PAC ilifanya ziara katika eneo la Mlimani City na kuutaka uongozi wa UDSM kurekebisha mkataba kati yake na kampuni ya Mlimani City Holding Ltd kutokana na mapungufu yaliyojitokeza, huku ikihoji sababu ya mwekezaji huyo kuja na mtaji wa Sh150,000 ( Laki moja na nusu ) tu.

Read 45 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli