We have 303 guests and no members online

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MPYA WA MWANASHERIA MKUU NA NAIBU WAKE.

Posted On Thursday, 01 February 2018 23:52 Written by
Rate this item
(0 votes)

Picha inayohusiana

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria mkuu wa serikali, pamoja na Paul Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali. Kabla ya uteuzi huo ulioanza Februari 1, Dkt.Kilangi alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) tawi la Arusha, na pia Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za mkondo wa juu ya mafuta-PURA.

Kwa upande wake Paul Ngwembe alikuwa Mkurugenzi wa masuala ya sheria katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania. Pia Rais amewateua aliyekuwa Mwanasheria mkuu wa serikali George Mcheche Masaju na Aliyekuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali Gerson Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama kuu.

Read 85 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli