We have 392 guests and no members online

WAVUVI MKOANI MARA WASALIMISHA ZANA HARAMU ZA UVUVI.

Posted On Friday, 02 February 2018 05:25 Written by
Rate this item
(0 votes)

Tokeo la picha la zana haramu za uvuvi

Zaidi ya wavuvi 80 wakazi wa kijiji cha Ruhu Muhundwe wilaya ya Rorya mkoani Mara, wamesalimisha nyavu haramu za uvuvi zipatazo 299 ambazo thamani yake imetajwa kuwa ni Shilingi milioni 33. Hatua hiyo imechukuliwa na wavuvi hao kufuatia doria inayoendeshwa katika maeneo mbalimbali ya ziwa Victoria. Afisa mtendaji wa kijiji cha Ruhu muhundwe amesema kusalimisha nyavu hizzo ni kutokana na jitihada zilizowekwa kukabiliana na uvuvi huo haramu.

Miongooni mwa zana nyingine zilizosalimishwa ni pamoja na kokoro 13 ambayo thamani yake ni milioni 7.8, kokoro za giza giza 9 zenye thamani ya milioni 9.9, pamoja na nyavu za makira 44. Aidha zoezi hilo limetajwa kuwa litakuwa endelevu ili kukabiliana na uvuvi haramu. Kaimu kamanda wa oparesheni haramu kanda ya ziwa Dk.Hassan Shelukindo pamoja na mkuu wa kikosi cha kudhibiti uvuvi haramu mkonani mara wameshukuru kwa kitendo cha kusalimisha zana hizo na kuwataka wanaojihusisha na uvuvi haramu kuacha mara moja kwani ni kwa manufaa ya Taifa. Zana zilizosalimishwa zimeteketezwa.

Read 39 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli