We have 359 guests and no members online

MMILIKI WA MELI YA BUAH NAGA 1 YA MALAYSIA ATOZWA FAINI YA MIL 770.

Posted On Friday, 02 February 2018 05:48 Written by
Rate this item
(0 votes)

Tokeo la picha la MELI YA BUAH NAGA 1

Picha na Michuzi Blog.

Waziri wa wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amekamata meli ya uvuvi mali ya Kampuni ya Buah Naga 1 ya nchini Malaysia na kuwatoza wamiliki wake faini ya Dola za kimarekani 350,000 sawa na Sh.milioni 770 kwa kosa la kukutwa na mapezi ya samaki aina ya papa yenye uzito wa kilo 90 bila miili yake, ambapo hiyo ni kinyume cha Kanuni ya 66 ya kanuni za Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu pamoja na kifungu cha18 (2) cha Sheria ya Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu ya mwaka 1998 na marekebisho yake ya mwaka 2007.

Meli hiyo ilikamatwa Januari 26 mwaka huu baada ya kufanyika ukaguzi uliosimamiwa na kikosi maalum cha kupambana na kudhibiti uvuvi haramu na utoroshaji wa samaki na mazao yake wakati ikifanya shughuli za uvuvi katika ukanda wa Bahari Kuu kati ya Mkoa wa Lindi na Mtwara. Pamoja na kukutwa na mapezi hayo ya papa, meli hiyo ilikutwa pia na bastola aina ya Bereta ikiwa na risasi 10 bila ya kuwa na nyaraka za umiliki wake.

Aidha, Waziri Mpina ameagiza fedha hizo zilipwe ndani ya siku saba huku akitoa onyo kali kwa wamiliki wa meli waliopewa leseni za uvuvi wa Bahari kuu kufuata masharti ya vibali vyao na katika zama hizi za utawala wa Rais, Dk.John Magufuli watachukuliwa hatua kali zaidi.

Kwa upande wa Kamishna wa Oparesheni wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya, Luteni Kanali Fredrick Milanzi amesema meli hiyo baada ya kukaguliwa imekutwa na mapezi kilo 90 ya samaki aina ya papa na bastola yenye risasi 10 ambayo inaendelea kushikiliwa na Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Mtwara hadi hati za umiliki zitakapowasilishwa.

Read 52 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli