We have 336 guests and no members online

MIGUNA MIGUNA, WAKILI ALIYEHUDHURIA KUJIAPISHA KWA ODINGA AKAMATWA.

Posted On Friday, 02 February 2018 11:44 Written by
Rate this item
(0 votes)

Tokeo la picha la miguna miguna

Wakili mmoja huko nchini Kenya ambaye alihudhuria hafla ya kujiapisha kwa kiongozi wa upinzani  Raila Odinga kuwa Rais amekamatwa na polisi mapema ijumaa hii. Wakili huyo Miguna Miguna, ambaye pia ni mshirika wa karibu wa Odinga aliyejitangaza kuwa kiongozi wa vuguvugu la National Resistance Movement (NRM), kundi ambalo wiki hii lilitajwa na serikali kuwa la kihalifu na kupigwa marufuku.

Miguna amekamatwa na polisi akiwa nyumabani kwake katika mtaa wa Runda jijini Nairobi. Kukamatwa kwake ni siku chache tu baada ya mbunge wa Ruaraka Tom Kajwang aliyesimamia zoezi la kumuapisha Raila Odinga kukamatwa ambapo jana alifikishwa mahakamani kwa makosa ya uhaini. Wakati huo huo Serikali ya Kenya imekitaja kitendo cha kiongozi wa muungano wa upinzani NASA, Raila Odinga kujiapisha kuwa kinyume cha sheria na kilichoweka hatarini maisha ya maelfu ya watu.

Read 59 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli