We have 367 guests and no members online

WAHAMIAJI 90 WAHOFIWA KUFA MAJI LIBYA.

Posted On Saturday, 03 February 2018 05:15 Written by
Rate this item
(0 votes)
Tokeo la picha la Ninety feared dead after shipwreck off Libya coast
Picha inayohusianaShirika la uhamiaji la kimataifa (IOM) limeripoti takriban wahamiaji 90 wamekufa maji baada ya boti yao kuzama katika pwani ya Libya. Baadhi ya wahamiaji walionusurika wamesema wengi wa wahamiaji hao walikuwa ni raia kutoka Pakistan. Katika taarifa za awali zilizoripotiwa na shirika la habari la Ufaransa RFI, zinasema watu watatu tu ndio wanaoaminika kunusurika. Katika kipindi cha miaka minne iliyopita Wahamiaji haramu zaidi ya 600,000 walifanya safari zinazoaminika kuwa za hatari kati ya Libya na Italia. Katika kipindi hicho, wahamiaji 6,624 waliingia Ulaya kupitia bahari ya Mediterranean, ambapo kwa mujibu wa shirika la uhamiaji la kimataifa, IOM, wengine 246 walikufa maji wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean.
Read 48 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli