We have 329 guests and no members online

MWIGULU NCHEMBA ASISITIZA UMAKINI KWA WATOAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA.

Posted On Saturday, 03 February 2018 10:19 Written by
Rate this item
(0 votes)
Tokeo la picha la MWIGULU NCHEMBA AKIWA TABORA
 
Watendaji wanaosimamia usajili wa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa wametakiwa kuwa makini katika zoezi hilo. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba wqakati akizungumza katika uzinduzi wa utoaji wa vitambulisho hivyo kwa wakazi wa Tabora, amesema umakini huo utasaidia vitambulisho hivyo kutotolewa kwa watu wasiostahili.
Waziri Nchemba amesema katika kipindi cha miaka ya nyuma wakati utaratibu wa kutoa vitambulisho hivyo haujaanza, baadhi ya raia wa kigeni walikuwa wakitumia mwanya huo kunufaika na huduma za kijamii kama elimu, ambapo baada ya kumaliza masomo walirejea katika nchi zao na kuzinufaisha kwa namna moja au nyingine ilihali wametumia pesa za watanzania. Katika kusaidia hilo amesema kila mwananchi anatakiwa kuwa mlinzi wa mwenzake ili kuhakikisha hakuna mgeni anayepenya na kupata kitambulisho hicho ambacho kitatolewa kwa wanachi bila malipo.

Kwa upande wake Andrew Massawe kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), amesema lengo ni kuhakikisha mpaka Desemba waka huuu, utoaji wa vitambulisho hivyo uwe umekamilika nchi nzima. Pia ametaja faida za vitambulisho hivyo kuwa ni kusaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi na wananchi kutambulika haraka wanapokwenda kupata huduma muhimu kama afya na elimu.

Read 53 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli