We have 361 guests and no members online

DRC; PADRI MMOJA ATEKWA NYARA NA MAAFISA WA POLISI.

Posted On Saturday, 03 February 2018 12:28 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image result for catholic church in drc

Chanzo, DW.

Jeshi la polisi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Jumamosi limetajwa kumteka nyara padri mmoja baada ya misa mjini Kinshasa kumalizika. Hayo yameelezwa na walioshuhudia wakati nchi hiyo ikiwa katika wasiwasi na mvutano mkubwa baina ya kanisa na serikali kuhusiana na hatua ya rais Kabila ya kukataa kuondoka madarakani. Mtawa mmoja alieyeshuhudia tukio hilo ameliambia shirika la habari la AFP kuwa Padri Sebastien alichukuliwa mateka na polisi muda mfupi baada ya kumalizika misa katika kanisa la parokia ya Mtakatifu Robert,

ambapo gari la polisi lilionekana katika maeneo ya kanisa hilo na baadae maafisa kadhaa wa polisi  waliteremka kwenye gari na kuanza kumpiga padri huyo.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa maafisa hao wa polisi walimsukuma padri huyo na kumuingiza ndari ya gari aina ya Jeep na kuondoka nae huku ikielezwa na watawa hao kwamba alikuweko mtu wasiyemfahamu aliyekuwa akichukua video ya padri huyo kupitia simu ya mkononi wakati misa ilipokuwa ikiendelea. Hata hivyo polisi imekataa kutoa maelezo yoyote kuhusu kisa hicho baada ya kutafutwa na shirika la  AFP.

 Tukio hilo limetokea katika wakati ambapo ni baada ya kuchukuliwa hatua kali na serikali za kuwaandama waumini wakikatoliki  kufuatia maandamano yaliyopangwa na kanisa hilo dhidi ya rais Kabila. Kiasi watu 15 wameuwawa kufikia sasa kutokana na hatua hiyo ya vikosi vya usalama iliyoshuhudiwa Desemba 31 na Januari 21 kwa mujibu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo Monusco. Rais Kabila mwenye umri wa miaka 46 amekuwa madarakani toka mwaka 2001 chini ya serikali ambayo inakosolewa kwa ufisadi,ukandamizaji na uzembe.Muda wake kwa mujibu wa katiba ulimalizika Desemba mwaka 2016  lakini ameendelea kubakia madarakani hali ambayo inasababisha umwagikaji damu katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo

Read 43 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli