We have 367 guests and no members online

MKUU WA MKOA RUKWA AAGIZA MKUU WA SHULE ACHUKULIWE HATUA.

Posted On Saturday, 03 February 2018 13:42 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image result for joachim wangabo

Joachim Wangabo Mkuu wa mkoa wa Rukwa, ameagiza mkuu wa shule ya sekondari Muhama manispaa ya Sumbawanga mkoani humo kuchukuliwa hatua za kisheria kwa tuhuma ya kuwatoza wanafunzi michango ya Sh5,000 kama gharama ya kuwapatiwa fomu za maelezo ya kujiunga na shule hiyo. Wangabo ametoa agizo hilo wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara kata ya Malangali baada ya baadhi ya wananchi kulalamikia jambo hilo, kwamba wazazi waemekuwa wakichangishwa pesa hiyo ili kugharamia fomuza kujiunga.

Aidha mkuu wa mkoa Bw. Wangabo amemhoji Hamidu Njovu Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga kuhusu uhalali wa mchango huo, lakini yeye alikana kulifahamu jambo hilo.
Hatua ya kisheria dhidi ya mwalimu huyo imekuja siku kadhaa baada ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Dkt. John Pombe Magufuli kusisitiza kuondolewa kwa michango kwenye shule mbali mbali za umma.

Read 54 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli