We have 344 guests and no members online

NIGERIA; JAJI ANAYESHUGHULIKIA WALA-RUSHWA, ATIWA MBALONI KWA KUPOKEA RUSHWA.

Posted On Sunday, 04 February 2018 07:50 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image result for Danladi Umar

Nchini Nigeria Jaji mmoja wa ngazi ya juu anayeshughulikia kesi za tuhuma za rushwa ameshatakiwa kwa kosa la rushwa hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa nyaraka za kimahakama nchini humo. Jaji huyo Danladi Umar anatuhumiwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini humo ya EFCC kwa kuomba rushwa kutoka kwa mtuhumiwa ya naira milioni kumi ambayo ni sawa na dola 27,800 ili aweze kutoa upendeleo kwa mtuhumiwa huyo hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa nyaraka za kimahakama ambazo pia zimeshuhudiwa na shirika la habari la AFP.

Taarifa hizo zimebainisha kuwa Jaji huyo anatuhumiwa pia kupitia kwa msaidizi wakre kuwahi kupokea rushwa ya naira milioni 1.8 mwaka 2012 kutoka kwa mtuhumiwa huyo kuhusiana na kesi hiyo. Umar ambaye pia ni mwenyekiti wa mahakama ya maadili mwaka jana alitupilia mbali mashitaka ya rushwa dhidi ya rais wa baraza la seneti nchini humo Bukola Saraki kosa analodaiwa kulifanya katika kipindi alipokuwa gavana wa jimbo moja nchini humo. Mashaka kuhusiana na uadilifu wa jaji Umar yamezidi kuongezeka wakati rais wa baraza la seneti nchini humo alipofutiwa mashitaka dhidi yake.

Read 32 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli