We have 355 guests and no members online

DRC: PADRI ALIYETEKWA NA POLISI AACHIWA HURU.

Posted On Sunday, 04 February 2018 08:11 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image result for Sebastien Yebo

Padri Sebastien Yebo wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Robert katika eneo la N'sele jijini Kinshasa- Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ameachiliwa huru jumapili hii. Padri huyo alitekwa siku ya jana Jumamosi na Polisi baada ya kuongoza misa ya asubuhi katika Kanisa hilo. Padri Yebo amezungumza na shirika la habari la RFI na kuthibitisha kuachiliwa kwake, lakini hakueleza hali ilivyokuwa baada ya kukamatwa.

Baada ya kuachiwa, Jeshi la polisi nalo halijazungumzia tukio. Baraza la Maaskofu nchini humo limelaani kukamatwa kwa Kasisi huyo na kusema kuwa halitachoka kuendelea kushinikiza mabadiliko ya kisiasa nchini humo. Mara nyingi kanisa Katoliki nchini DRC, limekuwa katika mstari wa mbele kupanga maandamano dhidi ya rais Joseph Kabila, wakimtaka ajiuzulu kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Desemba.

Read 62 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli