We have 372 guests and no members online

IMEBAINIKA, HITILAFU YA UMEME ILISABABISHA NDEGE KUANGUKA Z’BAR.

Posted On Sunday, 04 February 2018 09:46 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image result for NDEGE ILIYOANGUKA ZANZIBARNa Muungwana blog.

Ajali hiyo ilitokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume majira ya saa 7:00 mchana, wakati ndege hiyo ikijaribu kuruka, hitilafu ya mfumo wa umeme imetajwa kuwa chanzo kikuu cha ajali ya ndege ambayo ilisababisha vifo vya watu wawili juzi visiwani Zanzibar. Hata hivyo mbali na sababu hiyo, Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) cha Dar es Salaam, Dk. Bwire Rufunjo, almesema uchunguzi zaidi wa chanzo cha ajali hiyo unaendelea hata hivyo.


Dk. Rufunjo amesema katika hatua za awali wamebaini chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu katika mfumo wa umeme wa ndege kusabisha moto uliozaa mlipuko kutokana na ndege kuwa na mafuta mengi.
Alisema ndege hiyo yenye usajili wa 5H-TDF yenye uwezo wa kubeba abiria wanne ni mali ya NIT na ilikuwa Zanzibar kwa ajili ya matengenezo.
Mkuu huyo wa chuo.alisema, “Wakati ikiwa katika matengenezo, marubani wetu walikuwa wakiifanyia majaribio ili kuweza kufanya kazi yake ambayo ilikuwa kwa ajili ya ufundishaji wa wanafunzi wetu wanaochukua mafunzo ya urubani,”
Alisema waliofariki katika ajali hiyo ni Injinia Edger Mcha (26) na rubani Dominic Bomani (64) ambao ni wafanyakazi wa NIT. Daktari bingwa wa uchunguzi katika Hospital Kuu ya Mnazi Mmoja, Dk. Msafiri Marijani, alisema vifo vya watu hao vilisababishwa na kukosa hewa safi wakati ajali

Read 121 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli