We have 349 guests and no members online

WATU 13 WAMEKAMATWA NA ZANA ZA UVUVI HARAMU, KAGERA

Posted On Monday, 05 February 2018 06:10 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image result for UVUVI HARAMU

Watu 13 wanaodaiwa kutokea katika mwalo wa Kibale kata ya Kimwani Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, wamekamatwa kwa kosa la kujihusisha na uvuvi haramu katika kisiwa cha Mazinga kilichopo kata ya mazinga wilayani humo. Watuhumiwa hao waliodai kuwa ni vibarua tu na si wamiliki wa zana hizo, wamekamatwa Katika oparesheni ya kudhibiti uvuvi haramu inayoendeshwa maeneo mbalimbali ya ziwa Victoria. Zana zilizokamatwa ni pamoja na Makokoro 6 ambayo thamani yake imetajwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 6 na mitumbwi 6 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3.6.

 Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya Mazinga amesema serikali itahakikisha inafanya msako mkali kuanzia ngazi ya kijiji ili kuwatia nguvuni wamiliki halali wa zana hizo zilizokamatwa ambao wanadaiwa kutoroka. Emanueli Shelembi Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Muleba na mkuu wa wilaya ya Muleba Eng. Richard Riango wametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa serikali kwa kutoa taarifa za matukio kama hayo ili kuweza kudhibiti uvuvi haramu. Aidha mkuu wa huyo wa wilaya amesema oparesheni ni endelevu na inafanyika usiku na mchana. Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kuwa mashahidi wa wamiliki wa zana zilizokamatwa.

Read 44 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli