We have 373 guests and no members online

CCM KATA YA SOLA MKOANI SIMIYU, CHABAINI UJENZI WA CHINI YA KIWANGO.

Posted On Monday, 05 February 2018 06:47 Written by
Rate this item
(0 votes)

Related image

Viongozi wa CCM katika kata ya Sola wilayani Maswa mkoani Simiyu wamekagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya afisa mtendaji wa kata hiyo na kubaini ujenzi wa chini ya kiwango ikilinganishwa na kiasi cha pesa kilichotumika. Katika ukaguzi uliofanywa na katibu wa siasa na uenezi wa CCM wilayani Maswa Sita Mashala na viongozi wa chama hicho wa ngazi ya kata wamebaini uchakachuaji uliofanywa kwenye ujenzi huo uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 12, na hivyo kuagiza uchunguzi kufanyika dhidi ya mkandarasi aliyesimamia ujenzi wa jengo hilo.

Kwa upannde wake Masanja Mpiga diwani wa kata ya Sola amesema awali aliagiza uchunguzi kufanyika lakini hakuna hatua iliyowahi kuchukuliwa na viongozi wa ngazi za juu.

Read 37 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli