We have 155 guests and no members online

SHIRIKI KUPINGA VITENDO VYA UKEKETAJI KWA WANAWAKE.

Posted On Tuesday, 06 February 2018 10:47 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image result for FEMALE GENITAL MUTILATION

Dunia hii leo inaadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji kwa wanawake FGM inayolenga kuimarisha kasi kuelekea kumaliza utamaduni huo unaochukuliwa kimataifa kama ukiukwaji wa haki za binaadamu kwa wasichana na wanawake. Zaidi wa wanawake na wasichana milioni 200 wanakisiwa kufanyiwa ukeketaji wa aina mbalimbali huku kiasi ya wasichana milioni 44 wenye umri wa miaka 14 na chini ya hapo wakiwa wamekeketwa.

Image result for FEMALE GENITAL MUTILATION

Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu UNFPA pamoja na kwamba utamaduni huo unapungua katika mataifa mengi ambako ulienea mengi miongoni mwa mataifa hayo yanashuhudia idadi kubwa ya ongezeko la watu ikimaanisha kwamba idadi ya wasichana wanaofanyiwa ukeketaji itaendelea kuongezeka iwapo hakutaongezwa hatua za kukabiliana nao. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika kuadhimisha siku hii amesema "kwa heshima, afya na ustawi wa mamilioni ya wasichana walio hatarini, hakuna muda wa kupoteza. Kwa pamoja tunaweza kumaliza vitendo hivi viovu.

Read 47 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu